Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MLANDEGE: Hatutaki kuonewa, tutafika uwanjani

KIKOSI CHA MLANDEGE?fit=640%2C346 Mlandege

Sat, 18 Jul 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Timu ya Mlandege leo itashuka Dimbani mbele ya Kipanga katika uwanja wa Mao B Saa 10 :00 jioni.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa Mlandege kwavile wanataka kuendelea kuongoza Ligi kuu Zanzibar. nao Kipanga wanataka kujiweka katika nafasi ya juu.

Inaelezwa kuwa timu ya Mlandege inayoongoza ligi kuu Zanzibar kwa mujibu ya vyanzo vya habari timu hiyo ya mlandege haifanyiwi haki na wamuzi wanaopocheza .

Mtoa taarifa huyo hakupenda jinalake litajwe amesema kuwa “Timu yetu ya mlandege haifanyiwi haki katika mechi zake mbali mbali ilizocheza ,mfano tulipocheza na Jku penalt imekataliwa na baadhi ya mechi tunazocheza inaonekana baadhi ya matokeo yanapangwa”.

”Sisi kama Mlandege hata wakituonea , uwanjani tutakuja na tutaendelea kufanya vizuri kwavile vijana wana ari kubwa ya kushindana” ari yetu ya kuchukua ubingwa ipo pale pale.alisema Mtoa taarifa.

Chanzo: zanzibar24.co.tz