Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MICHEZO Rais wa TFF Karia ameguswa na taarifa za mtoto aliyefariki nje ya uwanja wa Taifa

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: --

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya kijana Ibrahim Hassan (7) aliyefariki nje ya uwanja wa Taifa Jumapili March 24, 2019 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya AFCON 2019 kati ya Tanzania dhidi ya Uganda.

.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema amepokea kwa huzuni taarifa za kijana huyo ambaye alikuwa na kiu ya kushuhudia mchezo huo, Karia amesema Shirikisho limeumizwa na tukio lililotokea na kusababisha mauti ya kijana huyo.

.

Kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na wapenzi wa soka kwa kumpoteza kijana huyo, TFF pia inatoa ubani wa kiasi cha Tsh Shilingi 500,000 kwa familia ya kijana huyo, kijana Ibrahim Hassan mwenye umri wa miaka 7 inaelezwa alifariki kwa kukanyagwa na watu baada ya kuanguka katika umatu iliyokuwa unataka kuingia uwanjani.

Chanzo: --