Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MECHI ZA CD 1 AGOSTO NA NAMUNGO KUCHEZWA TANZANIA

Capture 209.png?fit=532%2C340 MECHI ZA CD 1 AGOSTO NA NAMUNGO KUCHEZWA TANZANIA

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC zichezwe Tanzania.

Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.

Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

Chanzo: zanzibar24.co.tz