Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHAKAMANI: Walichosema TAKUKURU kuhusu nyaraka walizoomba kutoka kwa Aveva

730 Aveva TZW

Thu, 28 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa bado hawajakabidhiwa nyaraka walizoziomba kutoka kwa aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ili wapate nyaraka za upelelezi.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, pia upelelezi bado haujakamilika.

Pia Swai amedai kuwa bado hawajakabidhiwa nyaraka walizoziomba kutoka Ofisi ya Aveva ili wakamilishe upelelezi.

Hata hivyo, upande wa utetezi umeieleza mahakama kuwa wameipokea barua ya TAKUKURU kuhusu maombi hayo na wanayafanyia kazi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi January 11,2018.

KAMANDA MUSLIMU KUHUSU TATHMINI YA AJALI ZA BARABARANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

AGIZO LA MWENYEKITI WA UVCCM KWA VIONGOZI WALIOTEULIWA NA RAIS SERIKALINI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com