Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHAKAMANI: TAKUKURU wanaangalia jinsi ya kumhoji Aveva

1922 Aveva

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa inaangalia jinsi ya kumhoji Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na figo.

Mbali na Aveva mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Makamu Rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ambapo wanakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.

Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelekezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Pia amedai walishachukua maelezo ya mshtakiwa Nyange na kwamba wanaangalia jinsi ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza (Aveva) ambaye anaumwa kwa sasa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 8,2018.

Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.

BREAKING: SAID AMWAGA MACHOZI BAADA YA SCORPION KUHUKUMIWA MIAKA 7

Chanzo: millardayo.com