Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAHAKAMANI: Aveva aruhusiwa kutoka hospitali Muhimbili

2859 Aveva

Fri, 9 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva ameruhusiwa kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili.

Hayo yameelezwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa wakati shauri hilo lilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai amedai,  Aveva ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa maradhi ya figo.

Ameeleza kuwa wamepata taarifa kwamba Aveva amesharuhusiwa kutoka hospitalini, lakini ameshindwa kuletwa Mahakamani kwa sababu bado afya yake haijatengemaa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu, Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi February 22, 2018 itakapotajwa.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa mwingine ni Godfrey Nyange ambapo wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya March 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Kuhusu shtaka la kutakatisha fedha, Aveva anadaiwa kuwa kati ya March 15,2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 300,000 wakati akijua zimetokana na kughushi.

BREAKING: DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFIKA MAHAKAMANI KISUTU LEO



ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KESI YAKE NA HAMISA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com