Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lusajo: Niacheni najua ninachokifanya

Lusajo+pic Lusajo: Niacheni najua ninachokifanya

Mon, 31 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By CLEZENCIA TRYPHONE STRAIKA mpya wa KMC, Reliants Lusajo amewataka watu waendelee kufanya yao badala ya kumjadili yeye kwa kitendo chake cha kuachana na Namungo itakayoiwakilisha nchi kwenye mechi za kimataifa kwa madfai ukweli wote anaujua mwenyewe.

Mfungaji Bora huyo wa Namungo kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, amesajili na KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku aliyekuwa kocha wake, Hitimana Thierry akiumizwa kuondoka kwake, lakini akizungumza na Mwanaspoti straika huyo alisema anasikia kila kitu juu ya mashabiki kumshangaa kuihama Namungo na kutua KMC.

Alisema yeye ni mtu mzima na mwenye kujua kila analolifanya lina mustakabali gani wa maisha yake na famili kwa jumla, hivyo aachwe.

“Mimi najua malengo yangu, soka ni ajira yangu, sasa jiulize kwa nini nitoke timu inayoshiriki michuano ya kimataifa kisha nijiunge na KMC isiyoshiriki michuano hiyo?” alihoji Lusajo na kuongeza;

“Siwezi kuzungumza sana juu ya hilo, lakini mtu mwenye uelewa akitafakari atagundua sababu za kufanya uamuzi huu, pia nawaacha waendelee kuamini kile wanachoamini wao.”

Lusajo aliyemaliza msimu akiwa na mabao 12 akiwa na Namungo na kuiwezesha kumaliza nafasi ya nne mbali na kufika fainali ya Kombe la ASFC ikifungwa na Simba, alisisitiza anajua anachokifanya na anajivunia kwa kila kitu katika maisha yake ya soka.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz