Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lugola awaonya wanaolichezea jeshi la polisi

28902 LUGOLA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema jeshi la polisi lipo imara kupambana na uhalifu wa aina yoyote utakaojitokeza nchini na kuwataka watu hao kutothubutu kulichezea.

Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu polisi ili ziweze kufanyiwa kazi haraka kwa kuwa Serikali ya sasa si ya mchezo na imejipanga kikamilifu kwa kuwalinda raia wake.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Novemba 26, 2018 na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa Lugola ametoa kauli hiyo Jumamosi iliyopita katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Ragati, kata ya Kasuguti, jimbo la Mwibara, wilayani Bunda mkoani Mara.

Katika mkutano huo Lugola ambaye ni mbunge wa Mwibara amesema jeshi la polisi lipo imara na litaendelea kuwalinda wananchi pamoja na mali zao, ili polisi wazifanyie kazi zao kwa umakini zaidi na  wananchi wanapaswa kuwasaidia katika kufichua uhalifu katika maeneo yao wanayoishi.

Lugola alitoa kauli hiyo baada ya wananchi wa kijiji hicho kulalamika kuwa kuna kundi la vijana linaongozwa na mwananchi mmoja kijijini hapo linahatarisha amani na kusababisha  kuishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

“Polisi wapo kwa ajili yenu hivyo kuweni huru muda wowote kutoa taarifa za kiuhalifu katika maeneo yenu,” amesema.

“Kutokana na viashiria hivyo vya uvunjifu wa amani katika kata hii namuagiza mkuu wa polisi wilaya (OCD) kuwasaka, kuwakamata wale wote ambao wanahatarisha amani katika kata hii ya Kasuguti,” anasema Lugola.



Chanzo: mwananchi.co.tz