Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lugha yamfanya Chilunda kunyoa Bongo

15836 PIC+STARS TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

STRAIKA Shaban Chilunda anayeichezea CD Tenerife ametua nchini na kumuita kinyozi aweze kumkata nywele zake.

Mwanaspoti ambalo lilikuwa kambini hapo lilimshuhudia mshambuliaji huyo akinyolewa pembezoni ya chumba chake.

Mwanaspoti lilimuuliza sababu kubwa ya yeye kukata nywele zake nchini ndipo alipofichua kwamba Hispania anakuwa anakosewa kutokana na kushindwa kuelewana.

"Lugha ndio tatizo kule nikitaka kunyolewa hivi nanyolewa tofauti na ninavyotaka, ndio maana nimemuita kinyozi wangu aninyoe kwasababu ndio anaweza," alisema.

Aliongeza kwamba hatokuwa anarudi kunyia nchini lakini atajitahidi kujua lugha vizuri ili kupata mahitaji muhimu kama hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz