Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lipuli, KMC zatinga nusu fainali FA Cup

49176 Lipuli+pic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Lipuli na KMC zimekuwa timu za kwanza kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho(FA) baada ya kushinda mechi zao za jana jioni.

Lipuli iliifunga Singida United mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Samora Iringa sawa na KMC iliyoichapa African Lyon mabao 2-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo.

Katika mchezo wa Lipuli na Singida United, mabao ya washindi yalifungwa na kiungo Jimmy Shoji dakika ya 33 na beki Haruna Shamte dakika ya 90 kwa penalti.

Lipuli inasubiri mshindi kati Yanga na Alliance United ambazo zitacheza Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, KMC ilifunga mabao yao kupitia kwa Mohammed Rashid dakika ya 47 na Cliff Buyoya dakika ya 88.

KMC itacheza nusu fainali na mshindi kati ya Kagera Sugar itakayoikaribisha Azam katika mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Kocha wa Lipuli Selemani Matola alisema kutinga nusu fainali kwao ni hatua kubwa, hivyo watapambana kuhakikisha wanafika fainali na kutwaa ubingwa.

“Tunafurahi kupata ushindi kwani ni michuano ambayo tumewekeza nguvu kuhakikisha tunashiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani kama ilivyokuwa kwa Mtibwa Sugar,”alisema Matola.

Naye Kocha wa KMC, Ettiene Ndayiragije alisema vijana wake wamefanya kile ambacho amewaelekeza, hivyo anaamini wanaweza wakatimiza ndoto ya kutwaa ubingwa.

“Kila hatua ni ngumu tunasubiri tutacheza na nani kati ya Azam FC na Kagera Sugar, hivyo tunajipanga kuhakikisha tunafikia malengo ya ubingwa,”alisema Ndayiragije.

Timu hiyo inasubiri mshindi kati ya Kagera Sugar na Azam FC katika mchezo utakaopigwa Machi 26, 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz