Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lionel Messi apata mtoto wa tatu, FC Barcelona wampa zawadi ya kipekee

4581 DX8 TCQV4AABAXF TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana Machi 10, 2018 amepata mtoto wa tatu wa kiume aliyebatizwa kwa jina la Ciro.

Messi na familia yake wakiwa na Ciro

Kufuatia ushindi huo klabu ya Barcelona ambayo usiku wa kuamkia leo imepata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malaga, Kocha wa klabu hiyo, Ernesto Valverde amesema kuwa zawadi pekee ya Messi ni ushindi huo waliyoupata jana usiku kwani hakuna zawadi ambayo ingekamilisha furaha ya mchezaji huyo.

Nimeongea na Messi baada ya mchezo kumalizika, amesema anajiona mtu mwenye furaha zaidi kwa siku ya leo kwani mbali ya kupata mtoto lakini amefurahishwa zaidi na matokeo. Napenda kusema kuwa ushindi huu ni zawadi yake, hakuna zawadi nyingine kubwa kwa mchezaji wa Barcelona zaidi ya ushindi,“amesema Ernesto Valverde.

Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 15, na Philippe Coutinho, dakika ya 28 na kuifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa alama 72.

Chanzo: bongo5.com