Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi ya vijana ni kuchapana tu

Vijana Pic Data Ligi ya vijana ni kuchapana tu

Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LIGI Kuu ya Vijana chini ya miaka 20 kutoka timu 18 za Ligi Kuu inaendelea, huku vipigo na sare vikitawala.

Ikichezwa katika makundi matatu ya A, B na C ligi hiyo imekuwa na mvuto kutokana na matokeo ya kushangaza yanayopatikana katika mechi ambazo zimefikia raundi ya nne.

Katika matokeo ya ligi hiyo kwenye raundi ya nne mechi zilizopigwa Jumatatu wiki hii, Simba walipata ushindi wa kwanza kwa kuifunga Mbeya City mabao 2-0 baada ya kupoteza mechi mbili kwa kufungwa 1-0 na Tanzania Prisons kisha ikapigwa na 1-0 na Mtibwa Sugar kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na KMC.

Yanga baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Namungo, 2-1 dhidi ya Coastal Union, kufungwa 1-0 na Polisi Tanzania, juzi jumanne ililazimishwa sare na Ruvu Shooting.

Azam FC baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, 1-0 mbele ya Polisi Tanzania na suluhu 0-0 dhidi ya Namungo, jana iliingia uwanjani kucheza na Coastal Union - matokeo ambayo hayakupatikana hadi tunaingia mtamboni.

Mechi nyingine zilizochezwa katikati ya juma hili, Ihefu ilitoka sare ya mabao 2-2 na Prisons, Kagera Sugar ikashinda 2-1 dhidi ya JKT Tanzania, Mwadui FC ikaichapa Biashara United 1-0, Gwambina FC na Dodoma Jiji zilitoka sare ya 2-2.

Matokeo mengine KMC ililazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar, huku Namungo na Polisi Tanzania zikitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz