Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi ya Taifa Kabaddi ni hivi

Kabadi Pic Ligi ya Taifa Kabaddi ni hivi

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi ya taifa ya Kabaddi imesogezwa mbele hadi Februari 22-26.

Awali Ligi hiyo ilipangwa kuanza Januari 25 hadi 29 jijini Dar es Salaam kabla ya uongozi kueleza kuisogeza mbele kwa sababu za kiufundi.

Ofisa Habari wa Chama cha Kabaddi Tanzania (TKSA), Victoria Zambi amesema moja ya sababu za kusogeza mbele Ligi hiyo ni klabu kutokamilisha usajili wao,hivyo wamepewa siku saba kukamilisha.

"Sababu nyingine ni kufanya maandalizi zaidi ikiwamo kufuatilia wadau ambao walipelekewa barua za maombi ya kusaidia kufanikisha Ligi hiyo.

"Baada ya kusogeza tunaomba klabu zote zinazotarajia kushiriki zikamilishe usajili wao mapema Ili Kamati iweze kukamilisha maandalizi yake," amesema Victoria .

Amesema ligi hiyo, mbali na kutumika kusaka vipaji pia itakuwa mahususi kuteua kikosi cha taifa cha wanawake na wanaume watakaojiandaa na mashindano ya dunia badae mwaka huu nchini India.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afriks zilizofuzu kushiriki mashindano ya dunia baada ya kufanya vizuri kwenye yale ya Afrika mwaka jana nchini Misri.

Chanzo: Mwanaspoti