Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya kufunga goli 4, Neymar Jr azomewa na mashabiki wa PSG (+video)

1483 DTx0GU2UQAAlmHk

Thu, 18 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mshambuliaji wa Klabu ya PSG, Neymar Jr jana usiku ameshinda magoli manne lakini magoli hayo haikuwa sababu ya kushindwa kuzomewa.

Neymar Jr na Cavani

Neymar alifunga magoli yote lakini goli la nne ambalo lilikuwa la mkwaju wa penati alikataa kumuachia mshambuliaji mwenzake Edinson Cavani ambapo kama angeshinda penati hiyo basi angekuwa ndiyo mchezaji mwenye magoli mengi katika historia ya klabu hiyo.

Cavan ambaye mpaka sasa ana magoli 156 aliyoifungia klabu hiyo yupo sawa na mfungaji wa muda wote wa PSG, Zlatan Ibrahimovic ambaye naye ana magoli 156.

Kama Neymar Jr angemuachia penati kwenye mchezo huo wa jana, Cavan angekuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo.



Mashabiki wengi wa PSG walionekana jukwaani wakimzomea Neymar kwa kumuita mbinafsi kwa kitendo cha yeye kufunga magoli matatu lakini hakumuachia penati Cavan.

Kwenye mchezo huo wa jana PSG walishinda goli 8-0 dhidi ya vibonde klabu ya Dijon, mchezo huo ulikuwa ni wa Ligi kuu nchini Ufaransa (League 1) .

Chanzo: bongo5.com