Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewis Hamilton, hali mbaya msimu huu

Hamilton Verstappen (kushoto) akiwa na Hamilton (kulia)

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa mtetezi wa Formula 1, Lewis Hamilton bado anahali mbaya msimu katika harakati za kutetea taji lake.

Hamilton ameshaachwa kwa pointi 19 dhidi ya mpinzani wake mkuu, Max Verstappen (Red Bull) zikiwa zimesalia mbio 3 tu msimu huu kumalizika.

Wakati Mercedes wakihaha kutetea ubingwa wao, ubora wa magari ya mahasimu wao – Red Bull, umekuwa ni kitu cha utofauti kati ya timu hizi.

Lewis Hamilton mwenyewe alikiri, msimu huu Mercedes wana kazi ya ziada kutokana na ubora wa magari ya Red Bull.

Katika kuongeza maumivu kwenye kidonda, Hamilton amepigwa penati ya nafasi 5 kwenye mbio za Sao Paulo. Hii ni baada ya timu yake (Mercedes) kufanya mabadiliko ya injini ya gari analotumia dereva huyo.

Kwa sababu hiyo, Hamilton ataanzia kuanzia nafasi ya 6 kushuka chini na hii inaendelea kuweka rehani taji lake la F1 alilolitwaa msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live