Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewis Hamilton atunukiwa cheo cha heshima “Sir”

Lewis Hamilton Knighted Prince Charles Planetf1 Lewis Hamilton aliepiga magoti

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi mara nane wa mbio za langa langa “Formula 1” Sir Lewis Hamilton leo ametunikiwa cheo ch heshima na mwana mfalme Charles katika kasri la Windsor Castle.

Mwaka 2020, Sir Lewis Hamilton alikuwa ni mmoja ya watu waliopokea tuzo ya heshima kutoka kwa malkia Elizabeth II kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye mashindano ya F1 kwa kuitangaza vizuri nchi ya Uingereza.

Hamilton anajumuika na kina Sir Stirling Moss, Sir Jackie Stewart na Sir Jack Brabham kwenye ulimwengu wa mbio za Langa Langa kupokea heshima hiyo, ingawa Lewis ni dereva pekee ambaye bado anaendelea na mashindano ya F1 kutunukiwa.

Sherehe ya kumtunukia cheo cha “Sir” imefanyika leo Jumatano baada ya siku ya kadhaa kuisha kwa msimu wa F1, ambapo mbio hizo ziliisha kwa utata kwenye mbio za mwisho ambazo zilimfanya Max Verstappen kuibuka kidedea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live