Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewis Hamilton aonekana kukalia kuti kavu Mercedes

424 23824804 152648065350634 2728041756154134528 N TZW

Wed, 20 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Lewis Hamilton kwa sasa anaweza akawa hana furaha kubwa baada ya kitumbua chake kuonekana kuingia mchanga.

Dereva huyo wa magari ya mashindano ya Langa Langa kutoka Mercedes ameonekana kusambaza picha ya gari lake la kifahari aina ya LaFerrari kitendo ambacho kimekuwa kimezua maswali mengi.

Hali hiyo inatokana na kampuni ya Mercedes kuwa na upinzani mkubwa na Ferrari ambayo dereva wake katika mashindano ya magari ya Langa Langa ni Sebastian Vettel.

Gari la LaFerrari linatajwa kuwa na thamani ya kiasi cha dola milioni moja. Mastaa wengine ambao wanamiliki gari kama hilo ni Floyd Mayweather na Justin Bieber.

Chanzo: bongo5.com