Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leclerc, Verstappen kuwania Miami GP, Jumapili hii

F 1.jpeg Kwa mara ya kwanza F1 inafanyika katika Jiji la Miami Jumapili hii Mei 8, 2022

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raundi ya 5 ya mbio za magari yaendayo kasi Langa langa (Formula 1) msimu huu wa 2022, zinafanyika Jumapili hii Mei 08, 2022. Nchini Marekani jijini Miami ikiwa ni kwa mara ya kwanza mbiao hizi zinafanyika katika jiji hilo.

Kuelekea kwenye mbio hizi macho ya wengi yatakuwa kwa dereva wa Ferrari Charles Leclerc ambae ndiye kinara kwenye msimamo wa madera na bingwa mtetezi dereva wa Red Bull Max Verstappen ambaye anashika nafasi ya pili na katika mbio 4 zilizofanyika mpaka sasa maderea hawa kila mmoja kashinda mbio mbili.

Leclerc anaongoza kwa tofauti ya alama 27 dhidi ya Max anajumla ya alama 86, tofauti hiyo ya alama imekuwa kubwa kwa sababu Verstappen alishindwa kumaliza mbio za Bahrain GP na Australia GP kutokana na itirafu ya mfumo wa mafuta kwenye gari lake.

Lakini kwenye za Miami ambazo ni za 5 kati ya 23 za msimu huu itaangaziwa kama bingwa mara 7 wa Dunia Lewis Hamilton wa Mercedes Benz atafanya vizuri. Kwa sasa kwenye msimamo Hamilton yupo nafasi ya 7 akiwa na alama 28 na kwenye mbio zilizopita za Emilia Romagna zilizofanyika nchini Italia hakupata alama hata moja baada ya kumaliza wa 13.

Mbio za Miami zitakuwa na jumla ya mizunguko (Laps) 57 sawa na Kilomita 308.326 . Je dereva gani ataweka rekodi yakushinda mbio za kwanza za Miami Grand Prix? Weekend hii majibu yatapatikan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live