Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lebron James kuvunja rekodi ya Kobe Bryant NBA

LAKER LEBRONE Lebron James kuvunja rekodi ya Kobe Bryant NBA

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James yu mbioni kuvunja rekodi ya kibabe anayoishikilia gwiji Kobe Bryant ya kuwa mchezaji pekee kwenye historia ya NBA kufunga alama nyingi, alama 395 kwenye michezo mfululizo, michezo 16.

Lebron James amefunga alama nyingi, alama 383 kwenye michezo 15 mfululizo na kushika nafasi pili nyuma ya Kobe kwenye orodha ya wacheza mpira wa kikapu wa muda wote waliofunga alama nyingi zaidi kwenye michezo mfululizo.

Lebron huenda akaifikia rekodi hiyo kama akifanikiwa kufunga alama 12 lakini ataivunja rekodi hiyo kama atafanikiwa kufunga alama zaidi ya 12 kwenye mchezo wa Alfajiri  ya kuamkia kesho Disemba 25, 2021 dhidi ya Brooklyn Nets.

Kama Lebron atafanikiwa kuvunj arekodi hiyo basi atakuwa mwenye furaha zaidi, kwani Disemba 30 mwaka huu anatazamiwa kutimiza miaka 37 na kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na kuzidi kuwa mkongwe kwenye NBA.

Orodha ya wacheza kikapu waliofunga alama nyingi kwenye michezo mfululizo kwenye Historia ya NBA; 

1. Kobe Bryant - Alama 395, Michezo 16.

2. LeBron James -Alama 383, Michezo 15. 

3. Oscar Roberson - Alama 377, Michezo 12.

4. Dwyane Wade - Alama 314, Michezo 13.

5. Kevin Durant - Aama 299, Michezo 10. 

6. Shaquille O'Neal - Alama 272, Michezo 13. 

7. Russell Westbrook - Alama 241, Michezo 10.  

8. Dolph Schayes - Alama 239, Michezo 10.

9. Walt Bellamy - Alama 237, Michezo 9.

10. Richie Guerin - Alama 232, Michezo 9.

Chanzo: eatv.tv