Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LeBron James avunja rekodi ya ufungaji wa muda wote katika NBA

LeBron James Avunja Rekodi Ya Ufungaji Wa Muda Wote Katika NBA LeBron James avunja rekodi ya ufungaji wa muda wote katika NBA

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: Bbc

LeBron James amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa NBA, akipita rekodi ya Kareem Abdul-Jabbar ya miaka 39.

Nyota huyo wa Los Angeles Lakers James, 38, alifikisha pointi 38 katika kushindwa 133-130 na Oklahoma City Thunder na kuvuka alama ya Abdul-Jabbar ya 38,387.

Awali Abdul-Jabbar alivunja rekodi ya kufunga mabao Aprili 1984, miezi minane kabla ya James kuzaliwa.

"Kuweza kuwa mbele ya gwiji na mtu stadi kama Kareem, ina maana kubwa kwangu," alisema James.

James mwenye hisia aliinua mikono yote miwili kusherehekea huku Abdul-Jabbar mwenye umri wa miaka 75, ambaye alikuwa kwenye mechi katika uwanja wa nyumbani wa Lakers, alisimama na kupiga makofi.

Kulikuwa na mapumziko mafupi kwa ajili ya sherehe ya kuashiria mafanikio, huku James akichukua kipaza sauti ili kutoa hotuba fupi.

Chanzo: Bbc