Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lamine avunja ukimya Yanga

88909 Lamine+pic Lamine avunja ukimya Yanga

Wed, 18 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Yanga imeshinda vita ya kumbakiza beki wa kigeni Lamine Moro ikiwa ni siku chache tangu alipotishia kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Akizungumza jana, Lamine alisema amerejea nchini kujiunga na Yanga baada ya kumalizana na viongozi wa klabu hiyo.

“Nimerejea baada ya mambo yangu yote kuwekwa sawa kama ambavyo nilikuwa nataka, akili na nguvu naiweka kwa ajili ya timu ili kuipigania na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” alisema Lamine.

Meneja wa Lamine, Frank Chitambala alisema beki huyo wa kati ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

“Lamine amerejea baada ya kupata stahiki zake nawashukuru viongozi wa Yanga na wadhamini GSM,” alisema Chitambala. Beki huyo raia wa Ghana amecheza kwa kiwango bora mechi za Ligi Kuu Tannia Bara na kimataifa akicheza pacha na Kelvin Yondani.

Chanzo: mwananchi.co.tz