Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lamine, Niyonzima kuiboresha AS Kigali

NIYONZIMA 1 1?fit=800%2C534&ssl=1 Lamine, Niyonzima kuiboresha AS Kigali

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, beki Mghana Lamine Moro na kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima wamekutana tena AS Kigali na watacheza pamoja msimu ujao.

Lamine na Niyonzima wote waliachwa Yanga mwishoni mwa msimu ulioisha, Niyonzima akiwa ameitumikia timu hiyo kwa zaidi ya misimu nane huku Lamine akidumu kwa miaka mitatu.

Lamine amejiunga na AS Kigali kambini na anaendelea na mazoezi wakati akimsubiri swahiba wake Niyonzima ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda akitokea kikosini hapo.

Moja ya vigogo wa AS Kigali, ambaye hakupenda jina lake liwekwe wazi alisema usajili wa Lamine ni miongoni mwa sajili kubwa zilizofanywa na AS Kigali na wanategemea atawasaidia katika mechi za Ligi Kuu Rwanda (ARPL), sambamba na Kombe la Shirikisho Afrika.

“Lamine yupo Rwanda na tayari amejiunga na timu na anafanya mazoezi. Ni moja ya wachezaji wapya wanaopewa jicho la pekee kutokana na uzoefu wake ikiwa ni pamoja na kuichezea timu kubwa ya Yanga akiwa nahodha,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza;

“Wachezaji na benchi la ufundi limefurahia usajili wake na nzuri zaidi anakuja kucheza na Niyonzima ambaye wamezoeana hivyo naamini atakuwa na wakati mzuri hapa,” alisema.

Sambamba na hilo, kigogo huyo aliongeza timu yao ina imani kubwa juu ya Lamine na Niyonzima kutokana na viwango walivyonavyo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz