Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lamine, Banka wapangua kikosi Yanga

85417 Pic+lamine Lamine, Banka wapangua kikosi Yanga

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KURUDI kwa beki Lamine Moro na kiungo Mohammed Issa 'Banka' umepangua kikosi cha kocha Charles Mkwasa ambaye anaingia kwenye kibarua chake cha pili dhidi ya JKT Tanzania leo Ijumaa. Yanga wanawakaribisha Mafaande hao Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo unaoonyesha kuwa na upinzani kutokana kwamba kila timu inahitaji ushindi. Mkwasa ambaye anakaimu nafasi iliyoacha na Mwinyi Zaheara baada ya kutupiwa virago anatarajia kuiongoza Yanga kwenye mchezo wa pili wa Ligi akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda. Yanga inaikaribisha JKT Tanzania huku ikiwa na faida ya kurudi kwa wachezaji wao waliokuwa majeruhi ambao wanaweza kuwa na faida kikosini endapo watapata nafasi. Moro anaweza akapangua kikosi cha Mkwasa kwa kumuweka nje Kelvin Yondan aliyetoka kwenye majukumu ya timu ya taifa 'Taifa Stars'  ili kumpa muda a kupumzika huku Banka akipewa nafasi kubwa zaidi ya kucheza na kumuweka nje Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye inasemekana hayupo fiti zaidi. Akizungumzia mchezo huo Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema jukumu la kupanga timu ni la kocha huku akithibitisha kuwa Yondani baada ya kurejea amepewa muda wa kupumzika. Yondan alikuwa Stars nchini Tunisia walikocheza mechi ya pili ya makundi ya kuwania kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Libya na kufungwa bao 2-1. "Yondan pekee ndiye naweza kumzungumzia ambaye naamini pengo lake litazibwa kikamilifu na Moro ambaye amerudi baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha mwingine aliyerudi ni Banka huyo mwalimu ndiye atakayeamua aanze au akae benchi," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz