Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIVE: Rostam apinga ufadhili, umiliki Yanga

Video Archive
Fri, 21 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanachama na shabiki wa klabu ya Yanga, Bilionea Rostam Aziz amesema haungi mkono klabu hiyo kuwa chini ya mfumo wa umiliki wa mtu mmoja au kuendeshwa kwa kutegemea ufadhili.

Rostam ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari unaoendelea nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam.

Rostam hivi karibuni aliichangia Yanga Shilingi 300 milioni alisema iwapo timu itakuwa ikimilikiwa na mtu au kutegemea ufadhili, itapoteza maana na hadhi ya klabu hiyo.

"Kwa mtazamo wangu, Yanga haitakiwi kumilikiwa na mtu binafsi wala kutegemea ufadhili kwa sababu ni klabu yenye wanachama na mashabiki wengi.

“Yanga inatakiwa kumilikiwa na wanachama wake wote. Kunapokuwa na ufadhili au umiliki wa mtu binafsi unawanyima au kuwabinya wale walio wengi hivyo naamini Yanga inatakiwa ibakie kwa wanachama.”

“Ufadhili nao ni kama umiliki kwa sababu ufadhili ni mlango wa nyuma wa umiliki. Kwa sababu inawezekana kuna watu wanataka kuingia kwenye klabu, lakini wakahofia uwepo wako. Kwa hiyo huwezi kusema unapinga umiliki halafu wakati huohuo unasapoti ufadhili," alisema Rostam.

Pia Soma

Rostam alisema kiutaratibu, kila mwanachama wa Yanga anapaswa kuichangia klabu hiyo kulingana na uwezo alionao.

Chanzo: mwananchi.co.tz