Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwanini Ntibazonkiza haonekani Yanga?

NTIBAZONKIZA Kwanini Ntibazonkiza haonekani Yanga?

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amefafanua kwa kusema kuwa, kukosa utimamu wa mchezo na baadae kuitwa kwenye timu yake ya taifa ya Burundi ndiyo sababu za mshambuliaji wake Said Ntibazonkiza kutoonekana hivi sasa kwenye kikosi hiko.

Submitted by George David on Jumanne , 5th Oct , 2021 Nyota wa Yanga wa kimataifa wa Burundi, Said Ntibazonkiza akiwa kwenye mchezo wa Ligi kuu bara dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alifunga bao moja na kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Bumbuli amesema kuwa Ntibazonkiza, “Yupo na hakuna kinachoendelea kwa maana ya hiyo minong'ono, sasa hivi yupo kwenye timu ya Taifa kwasababu aliitwa timu ya Taifa”.

Bumbuli ameelezea kuwa, “Na wakati tupo Kagera tukapata call Up ya timu ya Taifa ameitwa Burundi na tukamruhusu kwamba aende Burundi kwasababu mechi iliyokuwa inakuja hapa hata kama angekuwa fiti asingekuwa sehemu ya mchezo”.

Afisa huyo wa Mawasiliano wa Yanga amewatoa hofu wanayanga na mashabiki wa nyota huyo kuwa, atarejea kikosini na kuitumikia Yanga mara baada ya kumalizia majukumu ya timu yake ya Taifa ya Burundi.

“Tunaamini atarejea na kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi. Natunaamini baada ya mchezo wao kirafiki atakuja kujoin na sisi Arusha maana timu inaondoka Jumatano kuelekea Arusha kwa ajili ya kambi ya siku 10".

Said Ntibazonkiza ambaye alisajiliwa kwenye dirisha dogo la msimu uliopita wa mwaka 2020-2021na kuonesha kiwango bora kilichopelekea kuwakosha wanayanga, kwasasa amepoteza nafasi kwenye kikosi baada ya ujio wa kocha Mohammed Nasreddine Nabi ambaye ameamua kumtumia Fei Toto kwenye nafasi ya nyota huyo.

Chanzo: eatv.tv