Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa tizi hili Yanga, Wanigeria watakula nyingi

Vita Yanga Kwa tizi hili Yanga, Wanigeria watakula nyingi

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STRAIKA mpya wa Yanga, Yusuph Athuman amesema aina ya tizi wanalopiga kambini kwao Avic, Kigamboni wale River United ya Nigeria hawachomoki kwa Mkapa Jumapili hii; “Yaani wakikoswa sana mbili.”

Yanga inarejea kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukosekana kipindi kirefu, baada ya mechi hiyo ya awali ya Ligi ya Mabingwa wikiendi hii watarudiana nchini Nigeria. Akizungumza na Mwanaspoti Athuman alisema kwa mazoezi ambayo wameyafanya mpaka sasa haoni kama wanaweza kumaliza mechi yoyote bila kupata bao. “Tupo kwenye mazoezi makali sana hiki ndio kipindi kigumu nilichokiona tangu nitue Yanga,makocha wamekuwa na ratiba ngumu sana lakini jambo zuri tumeongezeka ubora,” alisema Athuman.

“Tumecheza mechi mbili mpaka sasa ukiondoa ile ya kwanza dhidi ya Zanaco na binafsi naona timu inazidi kuimarika kwa kasi sasa kuna ubora unakuja. ““Eneo letu kama washambuliaji lina kazi nzito watu wanafunga sana unaona katika mechi zote tumefunga mastraika pekee na wote hakuna aliyefunga bao la kawaida unaona akili inatumika,”alisema staa huyo aliyenunuliwa kutoka Biashara United.

Aliongeza kuwa uwepo wa Heritier Makambo,Fiston Mayele,Ditram Nchimbi,Yacouba Sogne na yeye mwenyewe haoni kama Wanigeria hao watatoka salama na kwa uchache anaziona bao mbili na zaidi hazikosekani.

“Tumekuwa tunawaangalia hawa jamaa wanawachezaji wazuri baadhi lakini kwa mabeki wao kama tutakuwa tumekamilika hivi sioni kama tutakosa mabao mawili hapa au inawezekana ikawa zaidi ya hapo. ““Kila mshambuliaji amekuwa katika morali ya kufunga kutokana na ushindani haijalishi muda ambao unaingia Uwanjani kila mtu anataka kufunga.  

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz