Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa hili tatizo si Kaseja ni Manula

84820 Kaseja+pic Kwa hili tatizo si Kaseja ni Manula

Tue, 19 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. HIVI sasa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa Stars kuna ushindani kwa wachezaji wanaoitwa na wale ambao hawaitwi kuunda timu hiyo. Tangu kocha mkuu Etienne Ndayiragije akabidhiwe timu hiyo kama Kaimu Kocha Mkuu hadi sasa akiwa kakabidhiwa jumla, aliwahi kumwita kipa Aishi Manula wa Simba ingawa hakuitumikia hata mara moja baada ya kumwomba kocha huyo kukaa nje ya timu kwa sababu ya kujitibia na akiwa tayari atamjulisha, kocha huyo aliheshimu maombi ya kipa wake. Hadi sasa kuko kimya ingawa Etienne alitoa ufafanuzi Stars si timu ya mmoja bali nafasi ya Manula ipo na atamwita wakati wowote kwani anaendelea kufuatilia afya na maendeleo yake kisoka. Juzi Ijumaa wakati Stars ikicheza mechi ya kwanza ya Kundi J ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Guinea ya Ikweta na Stars ilishinda bao 2-1. Guinea ilikuwa ya kwanza kumtungua Kaseja, bao ambalo baadhi yao walidai ni makosa ya kipa huyo mkongwe huku wengi wakidai endapo Manula angekaa langoni basi Stars isingefungwa bao hilo lililoacha gumzo. Hata hivyo, makocha ambao wamewahi kuwafundisha makipa hao wawili kwa nyakati tofauti wamefafanua juu ya bao hilo na ni bao ambalo kipa yoyote ulimwenguni anafungwa hata angekuwa Manula. Idd Pazi aliyewahi kuidakia Simba na Stars miaka ya nyuma pamoja na kuwa kocha wa makipa wa Simba, alisema kwamba huu ni wakati wa Manula kutuliza akili na kuangalia wapi alikosea mpaka Kaseja amechukuwa namba. “Stars ingefungwa ikukweli ingeleta shida kwa Kaseja kutokana na aina ya goli alilofungwa, ni bao la kawaida ingawa kipa yoyote anaweza kufungwa. Kaseja alijiamini kwa sababu ya ukongwe na uzoefu wake pasipo kutarajia na wapinzani wangefunga. “Lakini Manula anapaswa kujichunguza wapi alikosea, hivi sasa kuna presha kubwa kwenye nafasi hiyo hasa mashabiki wa Simba ambao wanaona kipa wao haitwi kwenye kikosi hicho lakini hawajui, Manula alijisahau alivyokuwa hana mpinzani, hadi kufikia hatua kiwango kushuka. “Manula anapaswa sasa kujifunza na kuwa mtulivu zaidi kujifunza kwanini Kaseja amerudi Stars ambaye alisahaurika kabisa, ila ni kwa sababu amejitunza, anapambana na hakati tamaa, Kaseja hana muda mrefu wa kukaa Stars ninachoamini ni kwamba anatengeneza CV yake. “Hata hizi fainali sidhani kama langoni atakuwepo golini, hivyo hawa makipa wengine wanapaswa kujifunza kupitia Kaseja amepitia changamoto nyingi ambazo kwa mwingine angekata tamaa lakini sasa amerudi Stars akiwa kwenye ubora. “Endapo Manula atarudi kwenye timu hivi sasa bado atacheza kwa presha kubwa ya mashabiki kwani anaonekana wazi anahitaji utulivu wa muda mrefu na pasipo kushinikizwa kurudi kikosini na mashabiki,” alisema Pazi Pazi alisema Tanzania ina makipa wengi wenye vipaji lakini kwa asilimia kuwa hawapendi kuthamini vipaji vyao. “Makipa wapo wengi ila vijana wa sasa hawajithamini wenyewe, hivyo inakuwa vigumu hata kuwaendeleza, kujithamini sio kucheza tu bali hata nidhamu binafsi na ya mpira, hivyo kupitia hili alilolifanya Etienne kumuita Kaseja naamini wengi watajifunza, watu watambue mchezaji akifikisha miaka 40 ndipo wamuite mzee sio miaka 30 na kuanza kuwakatisha tamaa,” alieleza Kwa upande wa kocha wa makipa wa Mtibwa Sugar ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa makipa wa Stars, Patrick Mwangata alisema; “Mpira wetu mashabiki wana nguvu kuliko ufundi wa uwanjani, Manula amewahi kufungwa mabao mengi kama alilofungwa Kaseja. “Kiufundi bao lile hakuna kipa anayeweza kulikwepa, tatizo mashabiki wetu wanataka ushindi tu ndiyo maana inaonekana angekuwa kipa mwingine angedaka kitu ambacho si sahihi,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz