Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Yanga hii waleteni Gor Mahia

9368 Pic+yanga TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wawakilishi wa Tanza-nia Bara, Yanga wanahi-taji ushindi tu leo dhidi ya Gor Mahia ili kujihakikishia nafasi ya kuen-delea kubaki katika mbio za kuwania kufu-zu kwa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inaburuza mkia katika Kun-di D, ikiwa imefungwa mabao nane, bila ya kufunga bao lolote, lakini ushindi katika mchezo huo dhidi ya Gor Mahia utawafanya kufiki-sha pointi 4 na kujiweka vizuri.Mabingwa hao mara 27, wa Ligi Kuu Bara wanaingia katika mchezo huo wa marudiano wakiwa na sura tofauti katika kikosi chake baada ya kumal-iza tofauti zake na wachezaji wake pamoja na usajili wa nyota kadhaa.Yanga wamefanikiwa kumpa mkataba mpya beki wake Kelvin Yondani aliyeko-sa mechi ya kwanza kutoka-na na madai yake ya maslahi.

Habari njema zaidi kwa Yanga ni usajili wa msham-buliaji mpya Heritier Makambo kutoka FC Lupopo atakekuwa na jukumu la kumaliza ukame wa mabao katika mashindano hayo.Wakati Nkizi Kindoki Klaus kutoka Racing de Kinshasa ya DR Congo atachukua jukumu la Mcam-eroon Youthe Rostand aliyeruhusu mabao manane katika mechi tatu zilizopita.

Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema maan-dalizi waliyofanya yanatosha kuwafunga Gor Mahia na kupindua matokeo ya mechi ya kwanza.

Mwandila alisema kuongezeka kwa baadhi ya wachezaji ambao waliko-sekana katika mechi ya kwanza kutaongeza nguvu katika timu hiyo. Alisema wanakiu ya kupata ushindi wa kwanza baada ya kucheza mechi tatu bila ushindi na kushindwa kufun-ga hata bao. “Hatukuwa imara katika mechi za mwanzo kwani tulikuwa tukifanya makosa mengi lakini tumeyaona na kuyarekebisha hayo na jukumu lime-baki kwa wachezaji, “ alisema Mwandi-la.

Nahodha wa Yanga, Juma Abdul alisema wachezaji wenzake wote wan-amorali ya hali ya juu ili kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi.“Kuanzia kambini mpaka mazoezi kila mchezaji yupo na ari na morali kuhakikisha tunashinda kwa mara ya kwanza tukiwa nyumbani,” alisema Abdul.

Kocha Mwinyi Zahera anafa-hamu fika kwamba Yanga inatakiwa kuusaka ushindi kwa kila hali katika mchezo wa leo ili kufufua matumaini ya kupigania nafasi mbili za kuson-ga mbele kwenye michuano hiyo na kuepuka kurudia makossa ya kuishia hatua hiyo ya makundi.Mbali na hilo katika mchezo wa leo wachezaji walioongezwa kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu hiyo katika hatua hii watakuwa na nafasi ya kufan-ya hivyo huku pia wakijivunia sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao.Baada ya kumalizana na Gor Mahia katika mechi ya leo Yanga watabakiwa na mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya vinara wa kundi hilo USM Algier ya Algeria kabla ya kwenda kumaliza ugenini dhidi ya Rayon ya Rwanda.Katika matokeo ya mechi ya kwanza dhidi ya USM Algier Yanga ilitota kwa kufungwa mabao 4-0 kabla ya kuto-ka suluhu na Rayon kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kisha kupoteza ugenini kwa Gor Mahia.

Chanzo: mwananchi.co.tz