Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa Neymar, Messi anakaa, asema Cafu

100582 Neymar+pic Kwa Neymar, Messi anakaa, asema Cafu

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nyota wa zamani wa Brazil, Cafu amesema kutokana na uwezo alionao mshambuliaji wa PSG, Neymar, "hata Messi angekuwa nyuma yake" kutokana na ufundi wake. Mshajmbuliaji huyo wa Brazil ndiye mchezaji mwenye talanta kubwa ya ufundi duniani kwa sasa, anasema Cafu, kiasi kwamba hata nyota wa Barcelona, Lionel Messi anakuwa nyuma yake linapokuja suala la uwezo wakati mchezaji anapokuwa na mpira. Mshambuliaji huyo mwenye mchezo wa kuvutia amejijengea heshima ya kuwa mchezaji mwenye ubunifu wa hali ya juu katika soka duniani, inaandika yahoo.com. Kwa Neymar, mpira wa miguu ni aina ya burudani na ana uwezo wa kupita mabeki na kutengeneza nafasi ndani ya eneo la penati. Hayo pia yanaweza kuhusishwa na wachezaji wengine nyota duniani kama Messi, ambaye ameshatwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mara sita, lakini Cafu anaamini kuwa Mbrazili mwenzake ndiye mwenye sanaa ya kuchezea mpira kwa kiwango tofauti. “Kiufundi, Neymar ni mchezaji bora duniani," Gwiji huyo aliyetwaa Kombe la Dunia aliiambia Fox Sport. “Leo hii, kiufundi hakuna anayemzidi Neymar. Hata Messi, ingawa mimi ni shabiki wake. Lakini hamzidi kwa kuangalia ubora wa kiufundi.” Wakati uwezo wake hauna maswali, Cafu anakubali kuwa Neymar anatakia afanyie kazi uongozi wake. Gwiji huyo aliyekuwa nahodha wa Brazil wakati ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2002 alisema: “Leo sioni kiongozi yeyote ndani ya timu ya Brazil. “Leo sioni yeyote akimwambia haya Neymar: ‘Oh, usifanye hivi, fanya hivi. Hakuna! “Walimpa jukumu hilo na hajafikia huko. Si kwamba hataki, lakini ni kwa sababu si kada yake. “Umeshamuona akimshika Thiago Silva na Tite katika mazungumzo na kutatua tatizo? Hapana, si kada yake.” Wakati Neymar si aina ya mtu anayeweza kutoa amri kwa watu wanaomzunguka, ana uwezo wa kuwafurahisha kwa kutumia vitendo vyake uwanjani.

Chanzo: mwananchi.co.tz