Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuvujishiana Jezi Tunakoelekea Itakuwa Vita - Video

Video Archive
Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

KAIMU Msemaji wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga amegusia sakata la kuvuja kwa jezi zao kabla ya siku ya uzinduzi ramsi ambao ulikusudiwa huku akionekana kama vile kutupa dongo kwa watani zao wa jadi wakati alipokuwa akifafanua baada ya kuulizwa swali hilo na waandishi wa habari leo.

“Hili suala la jezi kuvuja sio jambo la ajabu, jezi za Chelsea na Man City zilivuja, nimeona kuna Watu wanashabikia jezi kuvuja, tuna Mwekezaji ame- invest Bilioni 2 kwenye jezi, inashangaza kuna Watu mashuhuri wengine Viongozi wanashabikia jezi kuvuja kitendo ambacho sio cha kiungwana.

“Mashabiki wa Simba wanataka jezi iwe jezi zilivuja hazilkuvuja kama jezi nzuri Watu watanunua, kuna Timu zimezindua jezi Mwezi huu hakuna jezi iliyovuja, imefika zamu ya Simba ndio kuna hizo fitna za ajabu za kuvuja kwa jezi ni tabia inayopaswa kukemewa, watu wa Simba watavaa jezi yao iwe imevuja au haijavuja.

”Tukianza utani wa jadi wa kuvujishiana jezi, utani wa jadi wa kufanyiana hujuma kwenye uchumi, tunapokwenda utakuwa sio utani wa jadi itakuwa ni vita,” Kaimu Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga.

Chanzo: globalpublishers.co.tz