Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumekucha Mbeya Tulia Marathon

Tulia Marathon Kumekucha Mbeya Tulia Marathon

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Zaidi ya wanaridha 4,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini wanararajiwa kushiriki mashindano ya mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 msimu wa nane zinazotarajiwa kufanyika Mei 10 hadi 11, mwaka huu katika viwanja vya Kumbukumbu vya Sokoine Jijini Mbeya.

Mashindano yatashirikisha mbio fupi na ndefu pamoja na zile za uwanjani huku yakiwa yamekuja kivingine kwa kushirikisha wanariadha kutoka mikoa mbalimbali nchini na mataifa ya nje.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust ambao ndio waandaaji wa mbio hizo, Joshua Mwakanolo amesema kwa sasa maandalizi yamenza vyema na wanatarajia mwitikio utakuwa mkubwa huku gharama za ushiriki kwa mbio fupi zikiwa Sh30,000 ilhali mbio ndefu ni 35,000.

Amesema Mei 10 washiriki watakimbia mbio fupi za mita 100, 200 800 mpaka 1,500 huku mbio ndefu zitakuwa za kilomita 5, 10, 21 mpaka 42 sambamba na kukabidhiwa zawadi kwa washindi.

Mwakanolo ametaja zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio fupi kuwa ni Sh500,000 ilhali wa pili 350,000, wa tatu 150,000 huku mbio za uwanjani mshindi wa kwanza ni Sh500,000, wa pili 300,000 wa tatu 200,000 wa nne na wa tano watapata Sh100,000.

Kwa upande wa mbio ndefu za kilomita 21 kutakuwa na washiriki watano huku mshindi wa kwanza atajinyakulia Sh1.3 milioni, wa pili Sh1 milioni, wa tatu 500,000 ilhali wa nne Sh 300,000 na wa tano 140,000.

Kwa upande wa mbio za ndefu za kilomita 42 washiriki watakuwa kumi huku mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Sh2 milioni, wa pili Sh1 milioni wa tatu 700,000 wa nne 400,000, wa tano 200,000 na washiriki watano wa mwisho watapata kitita cha Sh100,000 kila moja.

Mratibu wa mashindano hayo, Lwiza John amesema msimu huu utakuwa wa kipekee licha ya washiriki wa kitita cha fedha pia kutakuwa na medali mbalimbali ambazo zitatolewa.

Ofisa Michezo wa Jiji la Mbeya, Joyce Mwakifwamba amesema Serikali inaendelea kushirikiana na Tulia Trust sambamba na kuhamasisha wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo.

Chanzo: Mwanaspoti