Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kumbe John Bocco ana wababe wake!

11651 Pic+bocco TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Unaweza kusema mshambuliaji wa Simba, John Bocco ni tolu akiwa na futi sita na inchi mbili basi huyo ni mfupi unaambiwa, kuna huyu Mbelgiji, Kristof Van Hout amemzidi kwa inchi nane.

Hout mwenye urefu wa mita 2.98 ambaye ni kipa wa K.V.C. Westerlo ya Ubelgiji ndiye mcheza soka mwenye kimo kirefu zaidi duniani achana na Peter Crouch wa Stoke City ya England aliye na urefu wa futi sita na inchi saba.

Kipa huyo anayecheza ligi moja na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amekuwa akidaka kwa wepesi krosi na kona zinachongwa juu kutokana na urefu alionao.

Ukubwa wa umbile lake umekuwa ukiwatisha washambuliaji na muda mwingine hupoteza umakini pindi wanapokutana naye ana kwa ana, Hout pamoja na ubora wake wa kucheza mipira ya juu amekuwa wakifungwa kirahisi kwa mashuti ya chini.

Kuna wachezaji wengi wanaokaribia urefu wa Hout ambaye alizaliwa Februari 9, 1987 kwenye mji wa Lommel nchini Ubelgiji, Spoti Mikiki inakuletea nyota hao.

Paul Millar

Mscotland Millar aliyeachwa na Deveronvale FC anaurefu wa mita 2.07 (6 ft 9 in), nyota huyo wa amekuwa akicheza kama mshambuliaji na katika nafasi hiyo amekuwa na faida ya kufunga kwa wepesi mipira ya klosi na kona.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo ambaye pia amewahi kuzichezea Formartine United na Elgin City amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti yaliyomfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Vanja Ivesa

Ivesa ambaye anaichezea Istra 1961 ya Croatia, anaurefu wa mita 2.05 (6 ft 9 in) naye ni kipa kama ilivyo kwa kinara wa urefu Hout anayecheza ligi moja ya Ubelgiji na Samatta.

Kipa huyo mwenye uwezo wa kupangua mikwaju ya penalti ametumia miaka mingi kwenye uchezaji wake soka nchini Uturuki na klabu ya Eski?ehirspor ambayo ameichezea kwa miaka mitano.

Yang Changpeng

Changpeng wa HN Jianye ambaye wenzake wamempachika jina la Crouch wa China, anaurefu wa 2.05 m (6 ft 8 1?2 in), mshambuliaji huyo amewahi kutumia mwezi mmoja nchini England akiwa na Bolton Wanderers kwa majaribio ambapo hata hivyo alipoteza nafasi ya kujiunga na timu hiyo.

Lacina Traore

Muivory Coast Traore mwenye umri wa miaka 28 ni Mwafrika ambaye ameingia kwenye orodha ya kuwa miongoni mwa wacheza soka wenye kimo kirefu zaidi duniani.

Mshambuliaji huyo wa Monaco ambaye amekuwa akitolewa kwa mikopo mara kwa mara toka ajiunge na timu hiyo akitokea Anzhi Makhachkala ya Russia anaurefu wa mita 2.03 (6 ft 8 in).

Costel Pantilimon

Pantilimon wa Nottingham Forest ya England anaurefu wa mita 2.03 (6 ft 8 in), kipa huyo aliwahi kuwa chaguo la pili kwenye kikosi cha Manchester City nyuma ya Joe Hart.

Chanzo: mwananchi.co.tz