Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kukosa uzoefu kumetugharimu- Arteta

ARTETAA Kukosa uzoefu kumetugharimu- Arteta

Sat, 14 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Kocha wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amesema moja ya sababu ya kufungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa usiku wa jana dhidi ya Brentford kwenye ufunguzi wa msimu mpya wa EPL ni kukosa uzoefu kwa wachezaji wake vijana waliopo kikosini kwa sasa.

Arteta amesema hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 14, 2021 alipokuwa anafanya mahojiano na wanahabari punde tu baada ya mchezo huo kumalizika kwenye dimba la nyumbani la Brentford la Brentford Community, timu ambayo imepanda daraja msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 74 kupita.

Arteta amesema; “Sifikirii kama tulistahili tofuati na matokeo haya. Wachezaji wengi ni vijana wadogo na walikuwa wanajaribu kufanya kadri wawezavyo. Kwa baadhi yao ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kucheza ligi kuu, hilo linajieleza wazi kabisa.”

Maneno hayo yamepokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa Arsenal na kudai wachezaji wenye umri mdogo wasio na uzoefu wa EPL ni mshambuliaji Folarin Balogun aliyechukua nafasi ya Alexander Lacazette ambaye anasumbuliwa na homa na kijana mwengine ni kiungo Sambi Lokonga huku wachezaji 9 waliosalia wanauzoefu na michezo hiyo.

Kipigo hiko kimezidi kuonesha Arsenal kuhitaji zaidi maongezeko ya wachezaji wenye uzoefu na uwezo wa karba ya juu hususani kwenye dirish ahili la usajili lakini, Kocha Arteta alitupilia mbali uwezekani wa ‘Washika mitutu’ hao wa London kufanya usajili utakaochochewa na kipigo hicho kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa EPL wa mwaka 2021-2022.

Arteta amesema, “Sidhani kiwango cha leo kimeonesha kitu cha tofauti na ambacho tumewahi kukiona. Kipaumbele change kwa sasa ni kuwafanya wachezaji nilionao kuwa bora na kuanza kushinda michezo ijayo”.

Kwa upande mwingine, kocha wa Brentford, Thomas Frank aliyeweka historia ya ushindi wa kwanza wa EPL kwa timu hiyo iliyopanda kwa mara ya kwanza baada ya miaka 74 kupita na kufanya majaribio tisa yaliyofeli kuyapandisha daraja amesema mchango mkubwa ushindi huo umechagizwa na juhudi za mashabiki walioweza kutengeza ari na morali kwa wachezaji.

“Mazingira ya hali ya uwanja kutoka kwa mashabiki ilikuwa ya kushangaza sana. Ni kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu, tunafungua msimu na mashabiki zetu ambao baada ya ushindi huu wana ambao unatufanya tuwe kinara kwenye msimamo. Tutasherehekea kila ushindi lakini, tunataka kushinda zaidi”.

Hii ni mara ya pili mfululizo Arsenal kufungwa na Brentford, mara ya mwisho walikutana Juni 10, 2021 na Arsenal wakafungwa kwa mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki. Kipigo hiko kinawafanya Arsenal kushika mkia kwenye msimamo wa EPL, nafasi ya ishirini baada ya kuondoka bila alama kwenye mchezo huo huku kinara Brenford akiwa na alama 3.

Arsenal anataraji kuwa na kibarua kigumu kwenye michezo yake ijayo kwani amepangwa kucheza na mabingwa wa klabu bingwa Ulaya kwa sasa, Chelsea na kasha kucheza na mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City huku Brenford akijiandaa kuwavaa Aston Villa na Brighton Holve & Albion.

Chanzo: eatv.tv