Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufuzu CHAN2020: Taifa Stars, Sudan kupigwa Julai

45204 Stars+pic Kufuzu CHAN2020: Taifa Stars, Sudan kupigwa Julai

Fri, 8 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Sudan kati ya Julai 26-28, 2019 katika kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN2020 Ethiopia). Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limethibisha tarehe itakayofanyika michezo ya kusaka kufuzu kwa fainali za CHAN2020 kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambao safari hii utaingiza timu tatu mbili za kufuzu pamoja na wenyeji Ethiopia. Katika ratiba hiyo vijana wa Emmanuel Amunike wataanzia nyumbani kwa kuivaa Sudan kati ya Julai 26-28, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Taifa Stars itarudiana na Sudan jijini Khartoum kati ya Agosti 2-4, 2019, mshindi wa mchezo huo atasonga mbele na kucheza dhidi ya mshindi kati ya Kenya na Burundi mechi ya kwanza itachezwa Septemba 20-22, 2019 na marudiano itakuwa Oktoba 18-20. Tanzania imeshiriki fainali za CHAN mara moja tu mwaka 2009, ilipofanikiwa kuitoa Sudan na kufuzu kwa fainali hizo za kwanza zilizofanyika Ivory Coast. Wapinzani wa Tanzania katika kusaka kufuzu kwa Afcon 2019, Uganda Cranes wenyewe watacheza na Sudan Kusini kati ya Julai 26–28, 2019 na mechi ya marudiano itafanyika Agosti 2-4, 2019 Mechi zote mbili zitachezwa Kampala kwa sababu Sudan Kusini iliomba mechi zake zote za kimataifa mwaka huu zichezwe Uganda kwa kuwa Uwanja Juba upo katika marekebisho. Mshindi kati ya Uganda na Sudan Kusini atacheza na mshindi kati ya Somalia na Rwanda kati ya Septemba 20-22, 2019 na marudiano Oktoba 18-20. Timu 47, zinawania nafasi 15 za kuungana na wenyeji Ethiopia wa fainali za sita za mashindano ya CHAN. Uganda imecheza fainali nne za CHAN kuanzia ile ya Sudan (2011), Afrika Kusini (2014), Rwanda (2016) na Morocco (2018). DR Congo inashikiria rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili huku Morocco wakiwa mabingwa watetezi.

RATIBA NYINGINE Kanda ya Kaskazini Algeria Vs Morocco Tunisia Vs Libya

Kanda Magharibi – A Guinea Bissau Vs Mali Cape Verde Vs Mauritania Liberia Vs Senegal Kanda Magharibi – B:

Benin Vs Togo Raundi 2 Benin/Togo Vs Nigeria Niger Vs Ivory Coast Ghana Vs Burkina Faso

Kanda Kati: Raundi 2: Jamhuri Afrika Kati Vs /Chad Vs DR Congo Cameroon Vs Sao Tome and Principe Equatorial Guinea Vs Congo

Kanda Kusini: Raundi 2: Botswana/ Seychelles Vs Zambia Malawi/Swaziland Vs Angola Comoros Vs Namibia Madagascar Vs Mozambique Lesotho Vs South Africa Mauritius Island Vs Zimbabwe Raundi 3: Botswana / Seychelles Vs Zambia Vs Winner Malawi/Swaziland Vs Angola Comoros / Namibia Vs Winner Madagascar / Mozambique Lesotho / South Africa Vs Mauritius Island / Zimbabwe

Timu zitakazofuzu kutoka kila kanda: Kanda Kaskazini – timu 2 Kanda Magharibi A – timu 2 Kanda Magharibi B – timu 3 Kanda Kati – timu 3 Kanda Mashariki, kati – timu 2 + Ethiopia Kanda Kusini – timu 3



Chanzo: mwananchi.co.tz