Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Simba aonekana Uwanja wa Ndege Jomo Kenyatta

8925 Lechantre+pic TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kocha wa Simba, Pierre Lechantre na mtaalamu wa viungo, Mohammed Aymen wameonekana usiku wa kuamkia leo Ijumaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Hata hivyo, haikujulikana wapi wanaelekea lakini dalili zinaonyesha huu ukawa ndio mwisho wao baada ya kutokea kile kinachoitwa maelewano finyu baina ya Mfaransa huyo na msaidizi wake Masoud Djuma pamoja na kundi kubwa la viongozi wa Simba.

Awali jana baada ya sintofahamu ya alipo kocha wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, aliibukia jukwaani wakati mabingwa hao wakicheza nusu fainali ya Kombe la Mashindano ya Sportpesa SuperCups dhidi ya Kakamega Homeboys.

Akizungumzia uamuzi wa kutoka benchi hiyo jana, Lechantre alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa msaidizi wake Masoud Djoma kuonyesha uwezo wake.

Inasemekana kwamba Lechantre amekasirishwa na kitendo cha mabosi wa timu hiyo kumchunia kumpa mkataba mpya huku kukiwa na ukosoaji mkubwa wa namna timu ya Simba inavyocheza kwa sasa hivyo kuamua kuondoka.

Viongozi wa Simba wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah wameshindwa kuwa na majibu wa uhakika juu ya Lechantre huku wakidai kuwa watatoa taarifa kamili.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tulily ambaye yuko na timu hiyo mjini hapa alisema watatoa taarifa kamili baada ya mchezo huo wa nusu fainali wa jana ambao Simba waliibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalty 5-4.

Lechantre alijiunga na Simba mapema mwaka huu na kufanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu Bara walilokuwa wamelikosa kwa misimu mitano mfululizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz