Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Kimataifa wa Riadha afariki dunia

Kocha Wa Ridhaa Afariki Dunia Kocha wa Kimataifa wa Riadha afariki dunia

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Kimataifa wa riadha na aliewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGHU) Mzee Jasson Begashe amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne Januari 9, 2024 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanae Sixmund Begashe, marehemu Mzee Begashe atazikwa Ijumaa, Januari 12, Babati mkoani Manyara ambako ndiko alipokuwa akiishi.

Mzee Begashe ana mchango mkubwa kwenye riadha nchini, kwani aliliwezesha taifa kupata heshima kubwa kupitia wanafunzi wake wakiwemo wanariadha wa kimataifa, Juma Ikangaa, John Bura na wengine wengi.

Pamoja na mambo mengine Mzee Begashe mwaka 2010 aikiwa Kaimu Katibu Mkuu waĆ  TALGHU, atakumbukwa kwa ushirikiano wake mzuri na Serikali uliopelekea ongezeko kubwa kwa mishahara ya Watumishi nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live