Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha timu ya Riadha atoa neno

Felix Simbu Mwanariadha wa Tanzania,Felix Simbu

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha anaeinoa Timu ya Riadha iliyoshiriki michezo ya 32 ya Olimpiki Tokyo nchini Japan,Thomas John amesema kuwa maandalizi ya mashindano yajayo yaanze mapema ili kuwaandaa wanariadha wafanye vizuri zaidi.

John amesema hayo kupitia njia ya mtandao baada ya Wanariadha waliokuwa wanaiwakilisha Tanzania Kumaliza ushiriki wao katika mashindano hayo na kushika nafasi ya 7 kwa Felix Simbu huku mwenzake Gerald Geay, akishindwa kufika hata nusu ya mbio hizo yaana kilometa 21.1

Amesema Felix Simbu amefanya vyema licha ya kumaliza nafasi ya 7, kwa kuwa mbio zilikua ngumu sana na zenye ushindani mkubwa kiasi kwamba nyota kadhaa wenye viwango vya dunia wamechemsha na kushindwa kumaliza mbio hizo za kilometa 42.2

John akitoa mfano amesema, Ethiopia iliingiza wanariadha watatu, lakini wote walishindwa kumaliza mbio hizo, huku wakenya nao wakiingiza idadi kama hiyo lakini mmoja tu ndie alieshinda, mmoja akishika nafasi ya nne na mwingine akishindwa kumaliza.

Ametoa wito kwa wadau wa Michezo na hasa wale wa Riadha kujitokeza kusaidia riadha na sio kuliachia Shirikisho la Riadha na serikali peke yake.

Mwanariadha Felix Simbu alimaliza nafasi ya Saba (7) akitumia saa 2 dakika 11 sekunde 35 huku kinara wa mbio hizo Mkenya Eliud Kipchonge, akitumia saa 2 dakika na sekunde 38, na kuibuka kinara kwa kubeba medali ya Dhahabu.

Kwa upande wa Mshiriki mwingine kutoka Tanzania Gabriel Geay ,John amesema alijitoa baada ya kukimbia takriban kilometa 12.5 lakini alijitoa baada ya kuhisi maumivu makali ya mguu.Na kama angelazimisha kuendelea basi madhara yangekua ni makubwa zaidi, na pengine tungelazimika kumuacha Japan kwa ajili ya kupata matibabu.

"Tumemaliza mashindano salama,nimeingia kwenye top ten ya mbio hizi za olimpiki,nilidhamiria niweze kupambana ili nishinde medali lakini sijapata,kwa hiyo tunarudi nyumbani tuweze kujipanga kwa mashindano mengine kwa sababu haya yameshapita"amesema Simbu mara tu baada ya kumalizika kwa mbio hizo.

Timu hiyo inatarajia kurejea nchini Agosti 10 na Tanzania tulikuwa tukiwakilishwa na wanariadha watatu ambao ni Felix Simbu, Gabriel Geay na mwanadada Failuna Abdi Matanga alieshika nafasi ya 24 kwa mbio za Wanawake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live