Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mkuu Serengeti Boys atoa neno

13433 BOYS+PIC TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Oscar Milambo, amewasihi wadau na mashabiki wa soka nchini, kutowafananisha vijana wake na wachezaji wakubwa wa ndani au nje ya nchi.

Kocha huyo alisema kuwa hilo linaweza kuwaharibu vijana hao kisaikolojia wakavimba vichwa na kushindwa kuendeleza vipaji vyao.

Alisema binafsi amechukia kuona baadhi ya vijana wake wameanza kubandikwa majina ya wachezaji wanaotamba kwenye Ligi za Ulaya, kwa kuwa anafahamu madhara ya hilo kutokana na uzoefu wake tangu akiwa mchezaji hadi amekuwa kocha.

Akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya Rwanda wa kufuzu fainali za Afrika 2019 kutoka kanda ya Cecafa, alisema kwake yeye wachezaji wote wapo sawa na wanatimiza majukumu sawa ndio maana timu inapata ushindi.

“Hapana siwezi kusema Kelvin yupo juu ya Mkomola au chini, wala anafanana na mchezaji fulani anayeichezea timu fulani, sio jambo la kulizungumzia hivi sasa kikubwa ni kuhakikisha kwamba vijana wanafanya kazi kubwa ya kuisogeza timu kama ilivyokuwa kwa kaka zao kule Gabon,” alisema.

Tayari baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho wameshaanza kupewa majina ya wachezaji wa nje akiwemo mshambuliaji mahiri Kelvin John ‘Mbappe’, Agiri Ngoda na Jefferson Olivertwist ‘Kante’.

“Kiukweli siri yetu kufanya vizuri ni kujituma na kujali mazoezi, mfano sisi huwa tunaanza saa mbili lakini mimi huwa nafika saa moja asubuhi na kufanya programu yangu binafsi kabla ya kocha kufika, yeye akifika naacha yangu naungana na wenzangu hadi tunamaliza,” alisema mshambuliaji Kelvin John.

Aliongeza kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri na kuweza kuisadia timu kufika mbali ikiwemo kucheza Kombe la Dunia kwani hilo ndio lengo lao kubwa.

Alisema kuwa wanapambana kwa hali na mali, kuhakikisha mambo yanakuwa ili vijana watimize malengo yao ya kufanya vizuri katika medani ya kimataifa akimiani baadaye watachukua nafasi za kaka zao wa U-17 na watakwenda Kombe la Dunia la vijana mwakani.

Chanzo: mwananchi.co.tz