Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha atumia ndoto ya kucheza Ulaya kuivaa Enyimba Kombe la Shirikisho

81820 CAF+PI Kocha atumia ndoto ya kucheza Ulaya kuivaa Enyimba Kombe la Shirikisho

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Johannesburg, Afrika Kusini. Dan Maleselam kocha wa TS Galaxy ya Afrika Kusini anatumia uwezekano wa kupata mikataba ya kucheza soka barani Ulaya kuhamasisha wachezaji wake kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Enyimba nchini Nigeria kesho Jumapili. Pambano hilo la Daudi v Goliath ni moja ya mechi 16 za kwanza kati ya mbili zitakazoamua timu zitakazofuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika. Galaxy ni timu ya daraja la pili ambayo ilipata tiketi ya kucheza mashindano hayyo kwa kuiondoa Kaizer Chiefs katika fainali ya Kombe la FA, wakati  Enyimba imeshatwaa makombe manne ya CAF, yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika. Enyimba, klabu iliyotwaa mataji mengi nchini Nigeria katika mashindano ya klabu ya CAF, inategemewa kupata ushindi nyumbani mjini Aba kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa mwishoni mwa wikji ijayo. Lakini Malesela anaamini uwezekano wa kuingia hatua ya makundi ambao utawapa nyota yake nafasi ya kuonekana na mawakala wa klabu za Ulaya, unaweza kuipaisha Galaxy. "Kuvuka hatua ya mtoano itakuwa kitu kikubwa kwa sababu mechi hizo nyingi hufuatiliwa na mawakala wa klabu za barani Ulaya," alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 54. "Ingawa hatujaweka malengo yoyote katika Kombe la Shirikisho, kadri klabu itakavyoshiriki kwa muda mrefu ndivyo itakavyokuwa bora kwa kila mtu." Galaxy ndio klabu pekee katika timu zilizofikia hatua ya mtoano ambayo ina rekodi ya kushinda mechi zote nne, lakini ushindi katika mechi za nyumbani na ugenini ulikuwa dhidi ya timu ndogo kutoka Seychelles na Madagascar. Enyimba ni moja ya timu 16 zilizoingia michuano hiyo baada ya kuondolewa katika raundi ya mwisho ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa. Ilipoteza kwa idadi ndogo ya mabao ugenini na kufunga mabao matano bila ya majibu dhidi ya timu iliyojaa chipukizi ya Rahimo ya Burkina Faso kabla ya kutoka sare ya bila kufungana na kufungwa bao 1-0 na Al Hilal ya Sudan. Reuben Bala na Stanley Dimgba walifunga mabao mawili kila mmoja dhidi ya Rahimo nchini Nigeria, lakini Malesela haijaweza kufanya uchambuzi wa video za Enyimba. "Kwa kawaida sipendi kuangalia video za wapinzani kwa sababu inaweza ikawa kazi isiyo na maana," alisema. "Unaangalia timu na wiki moja baadaye wanakuwa na kikosi tofauti na staili tofauti."    Afrika Kusini na Nigeria zote zina wawakilishi wawili katika hatua hiyo, huku Bidvest Wits ikivaana ugenini na wababe wa Simba, UD Songo ya Msumbiji mjini Maputo wakati Enugu Rangers inavaana na ASC Kara ya Togo jijini Lome. Mechi za Kombe la Shirikisho Horoya (Guinea)    v Bandari (Kenya Yanga (Tanzania)    v Pyramids (Misri) Enyimba (Nigeria)    v TS Galaxy (RSA) A. Kotoko (Ghana)    v San Pedro (Ivory Coast) KCCA (Uganda)    v Paradou (Algeria) Gor Mahia (Kenya)    v DC Motema Pembe (Congo) Songo (Msumbiji)    v Bidvest Wits (Afrika Kusini) Elect-Sport (Chad)    v Djoliba (Mali) G. Eagles (Zambia)    v Hassania Agadir (Morocco) Cano Sport (GEQ)    v Zanaco (ZAM), Fosa Juniors (MAD) v Renaissance Berkane (MAR), Cote d'Or (SEY)    v Al Masry (Misri) ASC Kara (Togo)    v Enugu Rangers (Nigeria) Nouadhibou (MTN) v Triangle Utd (Zimbabwe) Al Nasr (Libya)    v Proline (Uganda) Generation (Sen)    v ESAE (Benin) -- Nasr inakuwa mwenyeji wa Proline katika jiji la Alexandria nchini Misri kutokana na hali ya usalama nchini Libya

Chanzo: mwananchi.co.tz