Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga awapiga mkwara Mwadui FC

28182 Pic+yanga TanzaniaWeb

Wed, 21 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa licha ya kuwakosa nyota wake wawili, Kipa Beno Kakolanya na Beki Kelvin Yondani lakini kikosi chake kipo fiti kuwavaa Mwadui Alhamisi na wala hana presha kabisa kutokuwepo kwa wachezaji hao.

Yondani na Kakolanya hawakuwepo katika kikosi cha Yanga kilisafiri mkoani Shinyanga juzi Jumanne na jana Jumatano katika msafara wa Kocha huyo wawili hao hawakuonekana.

Jana asubuhi  Kocha Zahera alitua jijini hapa akiwa na wachezaji watatu, Paul Godfrey, Abdalah Shahibu ‘Ninja’ na Kipa Ramadhan Kabwiri na kupitiliza moja kwa moja kuungana na wenzao Shinyanga.

Kabla ya kwenda Shinyanga kocha pamoja na wachezaji walikwenda kwenye ofisi ya Tawi la Mwanza Mjini kuwasalimia mashabiki na wanachama wa timu hiyo kisha wakaanza safari ya kuelekea wakiwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah.

Akizungumza kukosekana kwa nyota hao, Kocha Zahera alisema kuwa hiyo haiwapi presha katika mchezo wao wa Alhamisi na kwamba matarajio yao ni ushindi.

Akizungumza kwa kujiamini Kocha huyo alisema kuwa maandalizi waliyoyafanya kwenye Ligi Kuu si kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam pekee,bali walijipanga kila Mkoa kuhakikisha Yanga inapocheza inashinda.

“Hiyo haitupi presha,Yanga ni kubwa na ina kikosi kipana,hao wasipokuwepo inamaana nawapanga wengine,tumejipanga nje ya ndani ya uwanja wa Taifa,lazima tushinde mechi ya kesho(leo)”alisema Zahera.

Mkongo huyo alifafanua kuwa sababu ya kukosekana kwa wachezaji hao wawili ni kama wamefanya mgomo kwani baada ya mechi ya kimataifa,viongozi walipowatafuta walianza kuzima simu na baadaye walipofanikiwa kuwapata hewani wakasingizia kuwa na matatizo yao binafsi.

Alisema kuwa baada ya Benchi la Ufundi kubaini hizo njama,yeye kama Kocha Mkuu alishauri waachane nao na waondoke na wachezaji waliojitokeza kwenda mjini Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao.

“Mimi nimefika jana Jumanne  kutoka Kongo nilipokuwa na timu ya Taifa, lakini nilisikia hizo taarifa za Yondani na Kakolanya kugoma kusafiri, nilichosema ni kwamba wawaache sisi tutaenda na waliopo,”alisema Zahera.

Alieleza kuwa hata hivyo haimuumizi sana kichwa kuwakosa wachezaji hao kwani zipo baadhi ya mechi walizocheza bila kuwapo kwao na Yanga ikashinda hivyo na leo watapambana watapambana.



Chanzo: mwananchi.co.tz