Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga Aitahadharisha Kaizer Chiefs

Kocha Wa Yanga Luc Eymael?fit=700%2C400&ssl=1 Kocha Yanga Aitahadharisha Kaizer Chiefs

Tue, 11 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kocha Yanga Aitahadharisha Kaizer Chiefs May 11, 2021 by Global Publishers



ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, ameibuka na kubainisha wazi kwamba, wapinzani wa Simba, Kaizer Chiefs wanatakiwa kujiandaa kwelikweli kupambana na timu hiyo kwa sababu wakiichukulia kirahisi itawagharimu.

Mbelgiji huyo ameongeza kwamba, hilo linakuja kutokana na kasi ya Simba waliyonayo na pia mabadiliko makubwa ya timu hiyo huku Kaizer wakiwa hawaeleweki licha ya kuwa na nyota wengi wakubwa.

Kaizer Chiefs watakuwa wenyeji wa Simba katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali ambapo mechi ya kwanza itapigwa wikiendi hii nchini Afrika Kusini.



Eymael ambaye amewahi kufundisha nchini Afrika Kusini, amesema kwamba mechi hiyo itakuwa ngumu zaidi kwa Kaizer na wanatakiwa kupandisha viwango vyao kama watakuwa wanahitaji ushindi.

Mbelgiji huyo akaongeza kwamba, Kaizer wanatakiwa kubakia katika hali moja katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini kama wakiwa wanataka kutinga hatua ya nusu fainali ambapo ikiwa kinyume na hapo wanaweza wasifikie lengo lao.

“Simba inafanya vizuri tangu alipowasili kocha Didier Gomes na Milton Nienov, ambaye ni kocha wao wa makipa. Wana kikosi imara kuliko msimu uliopita na wana benchi zuri na wanacheza mpira mzuri.

“Kaizer sijui, hawana muendelezo mzuri, leo wanaweza kucheza hivi, kisha mechi ijayo wakawa chini, wanatakiwa kuwa na kiwango kimoja kama watataka kufanya vizuri mbele ya Simba.

“Kaizer wana wachezaji wazuri, naamini itakuwa mechi nzuri, wajue kucheza Dar es Salaam siyo kitu rahisi hata kidogo kwa sababu wenzao wanapata matokeo hapo na wanakuwa na mashabiki zao.”

STORI: SAID ALLY, Dar

Chanzo: globalpublishers.co.tz