Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba anena haya kuhusu kupindua meza

GOMEZ 1 Kocha Simba anena haya kuhusu kupindua meza

Tue, 18 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Kocha mkuu wa wekundu wa Msimbazi Simba, Didier Gomez Da Rosa amesema kuwa, licha ya kupoteza mchezo wa robo fainali ya kwanza kwa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, lakini bado ana imani kubwaya kufanya vizuri kwenye marudiano Mei 22, 2021.

Submitted by George David on Jumanne , 18th Mei , 2021 Kocha wa Simba, Didier Gomez Da Rosa.

Gomez ameyasema hayo muda mfupi baada ya kurejea nchini kutokea Afrika kusini kwenye mchezo huo akiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Gomez amesema, “Bila shaka tuna matumaini. Kwanza tunaamini tutashinda mchezo hicho ndico tunaweza kusema kwasasa, lkini wachezaji wamehamasika sana na wapo makini na tunapaswa tuweke matumaini yetu hai”.

Simba watakuwa na kibarua kizito cha kupindua matokeo ya 4-0 mbele ya Kaizer Chiefs kwenye dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi ya wiki hii Mei 22, 2021 na watalazimika kushinda utofauti wa mabao 5 ili kusonga mbele hatua ya Nusu fainali.

Chanzo: eatv.tv