KOCHA Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amewalaumu wachezaji kwamba hawakupambana kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli FC.
Katika mechi hhiyo timu hizo ziligawana pointi moja moja.
Katika mchezo huo, Simba walilazimika kufanya kazi ya ziada kusawazisha bao hilo kupitia kwa Mrundi Laudit Mavugo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juuko Murshid.
Akizungumza na gazeti hili, Lechantre alisema wachezaji wake walishindwa kujituma na kutoa nafasi kwa Lipuli kufanya wanavyotaka jambo ambalo liliwaweka kwenye wakati mgumu kusaka bao la kusawazisha.
“Mbinu walizoingia nazo Lipuli ndiyo ziliwachanganya wachezaji wangu wakashindwa kufuata maelekezo tuliyowapa na kucheza ovyo jambo lililowapa Lipuli kutawala mchezo na kupata bao lao kipindi cha kwanza; kipindi cha pili walitulia baada ya kuzungumza nao wakati wa mapumziko,” amesema Lechantre.
Baada ya mechi na Lipuli, Simba waliopo mbele kwa mechi tatu dhidi ya Yanga hawatakuwa na mchezo wowote mpaka Aprili 29 watakapokutana na wapinzani wao wakubwa Yanga mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.