Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba ajipa ubingwa mapema

58785 Pic+kocha

Tue, 21 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema leo ni siku maalumu kwa mashabiki wa klabu ya Simba kwa kuwa atatangaza ubingwa mbele ya Singida United.

Aussems ametoa kauli hiyo baada ya juzi kuilaza Ndanda ya Mtwara, mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Aussems alisema wametua mkoani Singida kutafuta pointi moja ili Simba kutangaza ubingwa ikiwa na mechi mbili mkononi dhidi ya Biashara United na Mtibwa Sugar.

“Natamani tujaze uwanja wao (Namfua), Jumanne itakuwa siku muhimu kwetu naamini tunakwenda kupata pointi tatu ambazo zitatufanya kutetea ubingwa wetu,” alisema kocha huyo.

Simba inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 88, Yanga nafasi ya pili (83) na imebakiwa na mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Azam.

Akizungumzia kiwango cha safu ya ushambuliaji, Aussems alisema imefanya kazi nzuri msimu huu na inastahili pongezi kutokana na idadi ya mabao waliyofunga.

Pia Soma

“Najisikia furaha kuona washambuliaji wangu wakifanya kile ambacho wanatakiwa kufanya kwa ufanisi mkubwa, japo kuna michezo huwa wanapoteza nafasi ila naweza kusema kiujumla wamefanya kazi nzuri,” alisema.

Simba ina pointi 88 ikiwa na mabao 74 ya kufunga huku Meddie Kagere akiwa amefunga 22. Emmanuel Okwi na John Bocco kila mmoja amefunga mabao 15.

Chanzo: mwananchi.co.tz