Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba Atishiwa Bastola Sauz

Matola2?fit=586%2C457&ssl=1 Kocha Simba Atishiwa Bastola Sauz

Tue, 18 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

UNAWEZA kusema siku ya balaa, haina mwenyewe! Ukiachana na Simba kufungwa mabao 4-0 yaliyoishangaza dhidi ya Kaizer Chiefs, kocha wake, Selemani Matola amekutana na dhahama ya kutishiwa bastola, tukio lililotokea nje kidogo ya Jiji la Johannesburg, hapa Afrika Kusini.

Matola alitishiwa bastola na vijana waliowavamia wakati wakitokea katika eneo la manunuzi la Mall Afrika, inayoaminika kuwa sehemu kubwa zaidi ya manunuzi barani Afrika iliyo katikati ya majiji ya Johannesburg na Pretoria nchini hapa.

Imeelezwa Matola alikwenda kufanya manunuzi ya baadhi ya vitu vya timu na kijana aliyembeba kwenye gari alikuwa ni rafiki yake.



Chanzo cha uhakika kutoka hapa Johannesburg, kimeeleza kwamba wakiwa njiani wanarejea hotelini katika eneo la Sandton, bado wakiwa njiani, gari moja liliwazuia na mmoja wa vijana hao alitoka akiwa na bastola mkononi, akawashusha chini Matola na dereva ambaye ndiye mwenye gari.

Baada ya kufanya hivyo, wababe hao wa Johannesburg maarufu kama Jozi waliondoka kasi na gari walilokuwemo kina Matola ikiwa ni baada ya kuwasachi na kuchukua vitu vingine walivyokuwa navyo.

Juhudi za kumpata Matola jijini hapa zimekuwa ngumu baada ya kutaka kuzungumza naye lakini ilionekana uongozi wa Simba haukuwa tayari kulizungumzia.

Mmoja wa Watanzania anayeishi hapa Johannesburg, amesema kijana aliyekuwa na Matola amewathibitishia kutokea kwa suala hilo na tayari ameripoti kwenye kituo cha Polisi ili kuhakikisha gari lake linapatikana.

“Ni kweli hili tukio limetokea, limetushtua sana. Lakini tayari liko polisi na wameanza kulifanyia kazi ingawa kwa hapa Johannesburg au Pretoria na Afrika Kusini kwa jumla, hili ni jambo la kawaida na washukuru kwa kuwa wamewaacha salama, maana vinginevyo yangekuwa mengine.

Watu huku ni wakatili sana kaka,” alieleza Mtanzania huyo ambaye ameishi Johannesburg kwa miaka 16 sasa.Jiji la Johannesburg ni moja ya eneo hatari sana katika masuala ya uhalifu na wageni wengi wamekuwa wakitakiwa kuwa makini wanapolitembelea.

Matola si mgeni na Afrika Kusini kwa kuwa amewahi kuishi wakati akiitumikia Super Sport United chini ya Kocha Pitso Mosimane ambaye sasa ni kocha wa Al Ahly ya Misri.Taarifa nyingine zinaeleza, wahusika waliwafuatilia kina Matola tokea wakiwa wameingia Mall of Afrika na kuna wakati walifanya mazungumzo nao kama watu wazuri ili kujua wataondoka baada ya muda gani ili waweze kutimiza uhalifu huo.

Simba inatarajia kurejea nchini muda wowote kuanzia leo ili kufanya mandalizi ya mwisho kuivaa Kaizer Chiefs katika mechi ya pili ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni baada ya kupoteza kwa mabao 4-0, juzi.

STORI NA MWANDISHI WETU, AFRIKA KUSINI | CHAMPIONI JUMATATU MEI 17, 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz