Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Rayon afichua sababu za Yanga kuibuka na ushindi

14498 PIC+RAYOR TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rwanda. Kocha wa Rayon, Mbrazil Roberto Goncalves amesema kama angekuwa na wachezaji wake tisa walioko nje ya timu hiyo angepata urahisi kuifunga Yanga.

Goncalves amesema wataingia katika mchezo wa kesho akiwa na kikosi chembamba baada ya kupoteza wachezaji wasiopungua nane.

Rayon itawakosa wachezaji wake watatu waliosimamishwa waliosimamishwa na CAF kufuatia vurugu katika mchezo dhidi ya USM Alger.

Wachezaji hao ni kipa wao namba mbili Kassim Ndayinga aliyefungiwa mechi mbili.kiungo Yannick Mukunzi mechi tatu na Chris Mbondi mechi mbili.

Pia itawakosa wachezaji Pierre Kwizera,Shasir Nahimana,Mohammed Hussein aliyetimkia Baroka FC wote wakimaliza mikataba yao na klabu hiyo.

Wengine waliomaliza mikataba na kutimka ni Faustin Usengimana aliyekwenda Qatar, Ismaila Diara Algeria  huku klabu hiyo ikimtimua kipa wao namba moja Ndayishimiye Jean kwa utovu wa nidhamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz