Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Pyramids aiwazia Azam FC

Pyramids 4 Kocha Pyramids aiwazia Azam FC

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa Pyramids FC ya Misri inayokipiga na Azam FC Jumamosi saa 9 mchana jijini Dar es Salaam, amesema wanacheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa.

Pyramids ambao wapo nchini tayari kocha wao, Ehab Galal alisema wameisoma Azam ni timu ambayo lazima kutumia akili kuikabili.

Pyramids FC ambayo misimu miwili iliyopita imefanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho, wamesajili kikosi ghali zaidi ya Azam Fc ambayo msimu huu imeonekana kujipanga upya.

“Tumeangalia mechi zao kadhaa, ni timu nzuri iliyojipanga na imara zaidi kuliko timu zote zilizofuzu hatua hii ya kwanza kutoka kule kwenye mtoano,” alisema kocha huyo ambaye kikosi chake thamani ya ukuta ni sawa na kikosi chote za Azam.

“Lakini lengo letu ni kushinda mechi zote mbili na kusonga mbele, msimu huu tunalitaka hili Kombe.

“Tunaelewa mazingira ya Dar es Salaam na tumejiandaa kupata matokeo chanya, kabla ya kurudi Cairo,” alisisitiza Kocha huyo mwenye presha kubwa ya kutakiwa kuipa Pyramids mafanikio

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz