Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Namungo awaambia Yanga hakuna kujuana huku

43557 Pic+namungo Kagere, Bocco ‘waharibu’ kibarua cha Pluijm Azam

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Yanga iko ugenini leo kuikabili Namungo FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) utakoafanyika kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi.

Kocha wa Namungo, Bakari Malima amewapiga mkwara Yanga kwa kuwaambia kuwa leo hakuna kujuana bali watacheza soka la maana na kupata ushindi.

Kocha huyo ambaye alikuwa beki wa zamani wa Yanga alisema anataka kujenga heshima kwa kushinda mchezo huo na kuingia hatua inayofuata kwani hata Namungo inataka kuwakilisha Tanzani Kombe la Shirikisho.

“Kule Yanga sawa nilicheza kwa wakati huo na kwa mafanikio ila sasa ni kocha nahitaji mafanikio kwenye timu yangu na kwa kuanza naanza na Yanga,” alisema.

Naye kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema wako vizuri tayari kwa mchezo huo na naamini watapata ushindi.

“Tunacheza na timu ambayo siifahamu lakini hatupaswi kuidharau timu yoyote kwa sababu kwanza tupo ugenini lakini lazima umweshimu mpinzani wako haijalishi ni timu ndogo au kubwa.

“Malengo yetu ni kushinda mchezo huo ili kwenda hatua inayofuata. Wachezaji wangu wako tayari kwa mchezo na naamini Mungu atatusaidia tutashinda,” alisema Zahera.

<.any() );

Chanzo: mwananchi.co.tz