Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mwadui FC achekelea sare Yanga

4578af36ac65b03049c10660f8bf2b32 Kocha Mwadui FC achekelea sare Yanga

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Mwadui FC, Khalid Adam anasema haikuwa rahisi kwa timu yake kupata pointi dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi.

Mwadui FC ilitoka sare na Yanga ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 68 na Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 na wote wamecheza michezo 36. Akizungumza baada ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Khalid alisema walicheza kwa tahadhari muda wote lakini walikosa umakini katika umaliziaji.

“Tulicheza kwa tahadhari, nashukuru nimepata pointi moja kuliko tungepoteza kwani tulitengeza nafasi lakini tulikosa umakini katika kumalizia,” alisema Khalid.

Alisema timu haiwezi kutengenezwa kwa msimu mmoja ila wanaendelea kupambana na anaamini timu yake itabaki ligi kuu kwani timu yake inacheza vizuri. Kwa sare hiyo Mwadui imefikisha pointi 41 katika nafasi ya 15 ikiwa na pointi sawa na Mtibwa Sugar na Alliance FC ambayo ilicheza jana na Simba na kufungwa 5-1.

Yanga walitangulia kupata bao lililofungwa na Feisal Salum Abdallah akimalizia pasi ya Mrisho Khalfan Ngassa lakini Mwadui walisawazisha dakika ya 56 kazi nzuri ya Yahya Mbegu akimalizia pasi ya Omary Daga. Naye mfungaji wa bao la Mwadui FC, Yahya Mbegu alieleza furaha yake baada ya kusawazishia timu yake kwenye mchezo huo.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuifunga Yanga, nina mfuraha sana,” alisema Mbegu.

Katika mchezo mwingine, KMC iliifunga Mtibwa Sugar bao 1-0, Namungo FC ikatoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons, Ndanda FC ikafunga bao 1- 0 na Mbeya City, Ruvu Shooting ikigaragazwa mabao 2-0 na Singida United, Biashara United ikatoka sare ya 1-1 na Coastal Union na Kagera Sugar ikachezeshwa gwaride na Polisi Tanzania la mabao 2-1

Chanzo: habarileo.co.tz