Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Milambo ajivunia ubora wa Serengeti Boys

48501 SB+PIC

Mon, 25 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema ubora wa vijana wake unaendelea kuimarika siku hadi siku kitu kinachompa jeuli ya kujiamini zaidi kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

Mirambo alisema ari ya wachezaji ipo juu baada ya kupata uzoefu wa mechi za kimataifa katika mashindano ya Uefa Assist kazi kubwa aliyonayo ni kusawazisha makosa yaliyojitokeza katika mashindano hayo.

Alisema wachezaji wameonyesha wako tayari kushindana katika fainali hizo zilizopangwa kuanza Aprili 14 hadi 28 kutokana na kufuata maelekezo ninayowapa siku hadi siku.

Mirambo alisema wachezaji wake wanaonyesha dhamira ya kupambana na wameahidi kufanya vizuri zaidi ili kuendelea kuipa heshima nchi yao.

"Tumecheza michezo ya kujipima na timu ya Azam B na timu za madaraja ya chini kwa kiasi nimeona mabadiriko na makosa mengi yaliyojitokeza kwenye mashindano ya Uefa Assist yamepungua naendelea kupambana kuhakikisha nakuwa na kikosi imara na bora kwa mashindano,"



Chanzo: mwananchi.co.tz